Joel 2:28-32

Siku Ya Bwana


28 a“Hata itakuwa, baada ya hayo,
nitamimina Roho wangu juu ya wote wenye mwili.
Wana wenu na binti zenu watatabiri,
wazee wenu wataota ndoto,
na vijana wenu wataona maono.

29 bHata juu ya watumishi wangu, wanaume kwa wanawake,
katika siku zile nitamimina Roho wangu.

30 cNami nitaonyesha maajabu katika mbingu
na duniani:
damu, moto na mawimbi ya moshi.

31 dJua litageuzwa kuwa giza
na mwezi kuwa mwekundu kama damu,
kabla ya kuja siku ya Bwana
ile kuu na ya kutisha.

32 eNa kila mtu atakayeliitia
jina la Bwana ataokolewa.
Kwa maana juu ya Mlima Sayuni na katika Yerusalemu
kutakuwepo wokovu,
kama Bwana alivyosema,
miongoni mwa walionusurika
ambao Bwana awaita.
Copyright information for SwhKC